Home Habari Mazungumzo Ya Mpango Wa Nyuklia Wa Iran Yaahirishwa

Mazungumzo Ya Mpango Wa Nyuklia Wa Iran Yaahirishwa

390
0

Duru ya tatu ya mazungumzo na Iran juu mpango wake wa nyuklia yaliyokuwa yanafanyika mjini Vienna, Austria yameahirishwa. 

Wajumbe wa Ulaya waelezea wasiwasi wao juu ya kujikongoja kwa mazungumzo hayo. 

Duru ya tatu ya mazungumzo na Iran juu mpango wake wa nyuklia yaliyokuwa yanafanyika mjini Vienna, Austria yaliahirishwa hapo siku ya Jumamosi. 

Lengo la mazungumzo hayo ni kuirudisha Marekani katika makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa makubwa sita.

Wajumbe wa Ujerumani, Ufaransa na Uingereza ambayo ni mataifa yaliyo sehemu ya mkataba huo wa nyuklia wamesema licha ya kwamba kila upande umeonesha utayarifu wa kuurejesha mkataba huo uliotiwa saini mwaka 2015, hatua zilizopigwa hadi sasa hazijafika mbali.