Home Habari Palestina Yaahirisha Uchaguzi Wa Bunge

Palestina Yaahirisha Uchaguzi Wa Bunge

197
0

Rais wa mamlaka ya ndani ya Palestina Mahmoud Abbas ametangaza kuwa uchaguzi wa bunge wa Palestina uliopangwa kufanyika mnamo Mei 22 umeahirishwa kwa muda usiojulikana. 

Abbas ametoa tangazo hilo baada ya mkutano na wawakilishi wa makundi kadhaa ya wapalestina mjini Ramallah na kusema uchaguzi huo hautafanyika hadi serikali yake itakapopata hakikisho kuwa eneo la Jerusalem Mashariki pia litashiriki kupiga kura.

Haijafahamika iwapo uchaguzi wa rais uliopangwa mnamo mwezi Julai ambao utakuwa wa kwanza tangu mwaka 2005 utaendelea au nao pia umeahirishwa.

Duru kutoka Palestina zinasema uamuzi huo unatokana na Israel kushindwa kuridhia matakwa ya mamlaka za Palestina za kuruhusu upigaji kura kufanyika pia kwenye eneo hilo la mji wa Jerusalem ambalo linakaliwa kwa mabavu.