Home Habari Zimbabwe Yashutumiwa Kukiuka Haki Za Binadamu

Zimbabwe Yashutumiwa Kukiuka Haki Za Binadamu

205
0

Vikundi vya haki za binadamu nchini Zimbabwe vinasema serikali imekuwa ikikiuka haki za kimsingi za watu tangu kuanza kwa ugonjwa wa COVID-19. 

Vikundi hivyo viliwasilisha uchunguzi wao katika mkutano wa njia ya mtandao na maafisa katika mji mkuu Alhamisi.

Katika mkutano huo, vikundi vya haki viliwasilisha ripoti wanayoiita Athari za COVID-19 juu ya Haki za Kijamii na Kiuchumi. 

Ripoti hiyo inaelezea jinsi serikali ya Zimbabwe ilivyokiuka haki za binadamu tangu kufungwa kwa shughuli za kiuchumi kutokana na COVID-19 kuanzia Machi 2020.

Calvin Fambirai, mkurugenzi mtendaji wa Chama cha Madaktari wa Haki za Binadamu wa Zimbabwe, alikuwa mmoja wa wasemaji. Anasema janga la COVID-19 liliangazia pengo la huduma ya matibabu kati ya wenye nacho na wasio nacho nchini humo.

Mara kadhaa, madaktari na wauguzi wa Zimbabwe wamegoma, wakidai vifaa vya kutosha vya kinga na mishahara bora wakati wa janga la corona.

Naome Chakanya, mtafiti katika Taasisi ya Utafiti wa Kazi na Maendeleo ya Uchumi ya Zimbabwe, alisema serikali lazima iongeze mishahara ya wafanyakazi wake wote ili kuwahamasisha

Serikali ilitangaza kufilisika kila wafanyakazi wake walipoomba kuangaliwa upya kwa mishahara yao. 

Watumishi wa serikali nchini Zimbabwe hupata chini ya dola 200 kwa mwezi. Mishahara ya wafanyakazi iliongezeka hadi angalau dola 500 kwa mwezi kupita kiwango cha umaskini.